Vyakula jamii ya maharage nikama vile maharage ya kawaida na yale ya soya, kunde, choroko, n.k. Virutubisho vya muhimu katika kundi la vyakula vya hapo juu ni wanga, protini na nyuzi nyuzi. Virutubisho vya ziada ni vitamini (kundi B) na madini.
Kwa ujumla, kiwango cha kinga (antioxidant) kilichomo kwenye maharage meusi ni mara kumi ya kile kinachopatikana kwenye matunda kama machungwa, zabibu na mengine. Hivyo unapokula maharage, siyo tu unapata ‘faiba’ ya kutosha bali pia unapata virutubisho muhimu mwilini kwa ajili ya kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya vinyelezi vya maradhi.
Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na ulaji wa maharage meusi kama ilivyothibitika katika tafiti mbalimbali za kisayansi;
MAHARAGE YANA KINGA DHIDI YA SARATANI
Utafiti umefanyika na kuthibitisha kuwa maharage meusi yana uwezo wa kutoa kinga mwilini dhidi ya saratani za aina mbalimbali.
MAHARAGE KINGA DHIDI YA UGONJWA WA MOYO
Utafiti ulionesha pia watu wanaokula chakula chenye kiwango kingi cha ‘faiba’ kama vile maharage, hawako hatarini kupatwa na magonjwa ya moyo, ikiwemo kiharusi.
MAHARAGE HUONGEZA NGUVU MWILINI
Ulaji wa maharage meusi husaidia kurejesha madini chuma mwilini na hivyo kuupatia mwili wako nguvu.
MAHARAGE YANA PROTINI NYINGI
Maharage yana kiwango cha juu cha protini bora mwilini, hivyo badala ya nyama nyekundu, ambayo ikizidi ina madhara mwilini, kula maharage meusi.
Hizo ndiyo faida za maharage mwilini ambazo kila mtu anapaswa kuzijua kwa faida ya afya yake ya sasa na ya baadae
Mapishi ya choroko
Mahitaji
Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima
Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia














No comments:
Post a Comment