Taswira hizi ni sehemu ya nyumba za maeneo ya Temeke Wailesi jijini Dar es salaam ambazo zimeshapata namba katika mpango wa kuwa na Post Codes kwa jiji hilo kuu la biashara nchini Tanzania. Inasemekana asilimia 70 wakaazi wa jiji hilo wanaishi katika maeneo yasiyopimwa. Mpango huu uliozinduliwa Septemba 14, 2012 una lengo la kurahisisha taarifa ya makazi ya watu kwa mitaa kupewa majina rasmi na nyumba kuwekwa namba.
PICHA KWA HISANI YA ISA MICHUZI.


















No comments:
Post a Comment