Tuesday, 28 January 2014

HOSPITALI YA AGAKHAN SASA KUTIBU SARATANI.

Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, imezindua mpango wa matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi.
Mpango huo umegharimu Sh130 bilioni.
Hatua hiyo imekuja huku ukiwa na ongezeko la watu wanaoumwa saratani nchini.
Wastani wa watu 44,000 wanagundulika kuwa na ugonjwa huo kila mwaka hapa nchini.
Akizindua mpango huo jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, alisema ugonjwa wa saratani umekuwa tishio kwa watu wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
Alisema tishio hilo linachangiwa na ukosefu wa matibabu na kuchelewa kugundua saratani.
“Mpango wa matibabu ya huduma za saratani kwenye Hospitali ya Aga Khan, utakuwa wa kwanza kwa taasisi binafsi za kiafya na jitihada hizi tunazipokea kwa mikono miwili na kwa pongezi nyingi kwa sababu saratani imekuwa tishio nchini,” alisema Dk Rashid.
Waziri Rashid alisema changamoto kubwa inayowakabili wagonjwa wa saratani, ugunduzi wa mapema kuhusu ugonjwa huo, matibabu na uhaba wa dawa.
Kwa mujibu wa waziri, wengi wanaanza tiba wakiwa wamechelewa.
Kwa upande wake, mtoto wa Aga Khan, Zahra Aga Khan, alisema dhamira kuu ya taasisi hiyo ni kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora za afya nchini na zenye kiwango cha kimataifa.
Alisema lengo la Aga Khan ni kujenga muunganiko wa kweli katika upatikanaji wa huduma bora za afya na kwa bei nafuu.
Huduma za saratani zitakazotolewa na Taasisi ya Aga Khan ni pamoja na kuweka vifaa vya upasuaji wa saratani, kuunganisha mtambo wa kinyuklia na CT Scan kwa ajili ya upimaji wa maradhi hayo
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!