Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.
Boti hiyo ilizama ikiwa imewabeba watu wengi kupita kiasi kinachotakiwa kwa uwezo wake.
Watu hao walikuwa wanakimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.
Mapigano yalianza Sudan Kusini mwezi December mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar kwa kuwa na njama ya kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo
No comments:
Post a Comment