Tuesday 24 December 2013

WATU WATANO WAMEFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI JIJINI DAR ES SALAAM

SONY DSC


Watu watano wamefariki dunia jijini Dar es salaam katika matukio matano tofauti likiwemo la kujinyonga katika tukio la kwanza kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Bwana Camilus Wambura amesema kuwa gari ambalo halikufahamika namba wala dereva wake limemgomba mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Asheri Mashaka mwenye umri wa miaka 51 katika eneo la Boko na kufariki papo hapo. Katika tukio la pili kamanda Wambura amesema wkuwa mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Godfrey Kimaro mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Kimara amekutwa amejinyonga kwa kutumia shuka chumbani kwake na sababu za kujinyonga hazijafahamika kwa kuwa hakuacha ujumbe wowote na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala. Katika tukio la tatu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke CP Elbert Kiondo amesema gari lenye namba za usajili T566CNZ Toyota Carina ambalo lilikuwa likiendeshwa na Sharif Mohammed mwenye umri wa miaka 27 limemgonga mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Seif Omar mwenye umri wa miaka 49 katika eneo la Tandika manispaa ya Temeke na kusababisha kifo chake papo hapo. Katika tukio la nne gari lenye namba za usajili T133CHN aina ya Scania Tipa amabalo lilikuwa likiendeshwa na Bwana Omar Said mwenye umri wa miaka 35 limemgonga mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la Omar Chikawe mwenye umri wa miaka 62 katika eneo la Temeka Mwembe Yanga na kusababisha kifo chake papo hapo baada ya kuteleza na kuingia chini ya uvungu wa gari hilo na miili yao imehifadhiwa hospitali Temeke kwa uchunguzi zaidi. Na katika tukio la tano mwanamke aliyefahamika kwa jina la Angela Thomas mkazi wa Chanika amekutwa amefariki chumbani kwake na chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!