Tuesday 24 December 2013

MKE WA BILLIONEA ALIYEJIUA KWA RISASI JIJINI DAR AIBUA MAZITO

MKE wa marehemu bilionea Suleiman Muhema, Zihija Muhema ametoboa siri kuhusiana na kifo cha mume wake aliyekutwa amefariki dunia kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya gari lake Kisarawe, Pwani.  
Akizungumza na paparazi wetu juzi, Zihija alisema kifo cha mume wake kimegubikwa na usiri mkubwa baada ya mumewe siku ya tukio kumwambia kuwa anamfuata mama yake aliko, hali ambayo ilimshitua kwa kuwa mama yake mzazi alishafariki siku nyingi zilizopita.


“Mume wangu alikuwa na siri kubwa  kwani baada ya kifo chake nimeamini kuwa kuna mambo mengi alifanya bila kunishirikisha.
“Hadi anakufa nilikuwa sijui kama anamiliki bastola, hali ambayo imenipa imani kuwa huenda chanzo cha kujiua alikuwa anakijua,” alisema.
Aliongeza kuwa siku ya tukio mume wake alimpigia simu na kumwambia ikifika saa 4.30 usiku ampigie simu na wakati huo ilikuwa ni saa 2.
Akasema kuwa alimjibu kuwa atakuwa amelala lakini alimsisitizia afanye hivyo na baadaye alisema anakwenda kujiua.

“Ilipofika saa nne usiku nilimpigia na kumuliza yuko wapi, aliniambia yupo kati ya Minaki na Kisarawe anakwenda kujiua hali ambayo ilinipa wasiwasi mkubwa.
“Nilipomuuliza kwa nini anataka kufanya hivyo? Aliniambia maelezo yote atayaacha polisi.

“Tuliendelea kuongea na mume wangu ili aniambie yuko wapi ili niweze kumfuata lakini akanijibu kuwa anamfuata mama yake alipo.
“Nilimuliza kama ni kujiua kwa nini aende mbali akajibu kuwa anaweza kuchukua maamuzi ya kujiua halafu asife hivyo anaona ni heri awe mbali na hospitali ili iwe kazi kupona kama ataenda kuokolewa.

“Nilimuliza tena sababu ya kujiua, alikata simu. lakini kabla ya hayo yote nilimuuliza akifa tukamzike wapi? Akajibu Dar karibu na watoto wake,” alisema mke huyo.
Uchunguzi wa gazeti umebaini kuwa marehemu aliwahi kulalamikiwa na mkewe huyo Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar kuwa alimtishia maisha na likafunguliwa jalada lenye kumbukumbu namba  OB/RB/12734/2013, Julai 20 mwaka huu.

Hata hivyo, jalada hilo lilifungwa Agosti 5, mwaka huu baada ya wanandoa hao kuelewana.
Mke wa marehemu alipoulizwa kuhusu hilo alikiri na kusema katika ndoa mambo kama hayo yapo  na waliyamaliza.

Akizungumzia mali za marehemu, mama huyo alisema hivi sasa kuna maneno mengi yanasemwa kuhusu magari makubwa, akasema yapo na hayajapotea ambapo ni Scania namba T 793 CHE, T 159 CGF na  T 331 CHK ambayo aliyanunua yeye (mke) lakini alimkabidhi mumewe kusimamia.

“Ninasikitika kusikia kuna watu wanaosema vibaya, kama ni ndugu wa marehemu wafike kuniona kwa ajili ya kuwekana wazi,” alisema.

-gpl 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!