Friday 27 December 2013

TASWIRA KATIKA MAZISHI YA MWANAFUNZI WA CBE ZEINABU J KASENGA ALIYEFARIKI JUZI DEC 23:

MAREHEMU ZEINABU J KASENGA
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi CBE Dodoma Mhe, Remidius M. Emmanuel alishiriki kwenye mazishi ya marehemu Zeinabu J. Kasenga katika makaburi ya Wahanga (maili mbili) mnamo tarehe 24/12/2013.


 Shekhe akimuombea Dua marehemu katika kaburi lake.
 Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi (COBESO)  walishiriki na wadau mbalimbali wakiongozwa na Rais na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe, Dickson Msigwa (katikati) katika picha hii.

 Watu walioshiriki kwenye mazishi
 Mawaidha ya kitolewa na shekhe (Hakuna anayejua siku wala saa kukutwa na umauti, cha msingi ndugu zangu tujiandae, shukuru Mungu ukiona jua linavyochomoza lakini inawezekana usione linavyo zama. Siku zote kifo hakizoeleki) maneno ya Shekhe

 Wadau wakiwa na Rais wakizungumza jinsi msiba huu ulivyo wagusa, Mmoja wao akisema chanzo cha kifo hicho ni maji, mnamo December 23 marehemu na marafiki zake walienda kuogelea African Dream baada ya kuogelea ndio akazama kama baada ya dakika mbili ndio kupata msaada wa kutolewa na kupelekwa Hospital General, mnamo usiku wa kuamkia December 24 akapotea maisha yake.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!