Sunday, 1 December 2013

PAUL WALKER STAR WA FAST AND FURIOUS AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA GARI




Shabiki wa filamu kubwa duniani Fast and Furious atakuwa sio mgeni
 wa kazi za star Paul Walker. Huyu ni kijana aliyepata umaarufu mkubwa
 kupitia
kazi zake za uigizaje kwenye filamu za Fast and Furious na nyingine.

Story ya kifo chake imechukua nafasi kubwa kwenye mitandao leo
 na zinasema kuwa star huyu alikuwa anatoka kwenye shughuli ya
 kuchangi  watu kupitia  organisation yake ya Reach out World Wide.

Paul Walker alikuwa na mwenzake ambaye ndio aliyekuwa dereva wa gari
 la kifahari aina ya Porsche Carrera GT na wakiwa njiani kurudi nyumbani
 ndio dereva akapoteza control ya gari na kugonga nguzo ya taa uliokuwa
 pembeni mwa barabara.
 Hii ndio gari aliyopata nayo ajali na picha ilipigwa saa chache kabla ya kifo
 chake.
Hapo unaona 
gari ilivyo gonga nguzo na kukatika kati kati.

Habari pia zinasema baada ya gari kugonga nguzo ya taa lika waka 
moto mkubwa uliopelekea kifo cha Paul aliyefariki akiwa na  miaka 40.

Paul ameacha mtoto wa kike wa miaka 15.

Kifo cha Paul kitapelekea mauzo makubwa ya filamu zake ikiwemo
 Fast and Furious.
Hapo Paul Akiwa Na mtoto wake kike.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!