Pages

Wednesday, 6 November 2013

TAASISI YA WAMA INATARAJIA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA NA UTEPE WA PINKI UTEPE MWEKUNDU KUKABILIANA NA UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NA MATITI


img_0858

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kushirikiana na Utepe wa Pink Utepe Mwekundu (PRRR) wanatarajia kuanza kufanya kazi kwa pamoja ya kuhakikisha kuwa ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti unapungua  au kuisha kabisa hapa nchini .
Hayo yamebainishwa leo wakati wa mazungumzo baina ya Wafanyakazi wa Taasisi ya WAMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Ujumbe kutoka Utepe wa Pinki Utepe Mwekundu yaliyofanyika katika ofisi za  WAMA zilizopo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Utepe wa Pinki Utepe Mwekundu Dk. Doyin Oluwole alisema  jambo la muhimu ni kuangalia jinsi gani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja na kuweza kuudhibiti ugonjwa huo ambao unawatesa wanawake wengi hapa nchini.
“Ili kukabiliana na  ugonjwa huu  Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa dharula wa kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)  na Ukimwi (PEPFAR)imetoa  dola za kimarekani millioni tatu kwa kipindi cha miaka mitano na mashine 16 za cryotherapy kwa ajili ya kusambaza huduma za upimaji na tiba kwa wanawake wenye ugonjwa saratani ya shingo ya kizazi”, alisema Dk, Doyin.
Pia kwa kipindi cha miaka mitatu  Shirika la Misaada la Marekani (UNAIDS) limetoa dola 33,000 kwa ajili ya kusaidia ushiriki wa wanawake wenye VVU na kufanya kazi na vikundi vidogovidogo katika jamii. Taasisi ya Bristol –Myers Squibb kwa kipindi cha miaka  mitatu imetoa dola za kimarekani milioni 1.2 kwa ajili ya kusaidia huduma za kuhamasisha jamii kuhusu  vikoba na kuimarisha huduma za jamii

No comments:

Post a Comment