Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kushirikiana na Utepe wa Pink Utepe Mwekundu (PRRR) wanatarajia kuanza kufanya kazi kwa pamoja ya kuhakikisha kuwa ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi na matiti unapungua au kuisha kabisa hapa nchini .
Hayo yamebainishwa leo wakati wa mazungumzo baina ya Wafanyakazi wa Taasisi ya WAMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Ujumbe kutoka Utepe wa Pinki Utepe Mwekundu yaliyofanyika katika ofisi za WAMA zilizopo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Utepe wa Pinki Utepe Mwekundu Dk. Doyin Oluwole alisema jambo la muhimu ni kuangalia jinsi gani wanaweza kufanya kazi kwa pamoja na kuweza kuudhibiti ugonjwa huo ambao unawatesa wanawake wengi hapa nchini.
“Ili kukabiliana na ugonjwa huu Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa dharula wa kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi (PEPFAR)imetoa dola za kimarekani millioni tatu kwa kipindi cha miaka mitano na mashine 16 za cryotherapy kwa ajili ya kusambaza huduma za upimaji na tiba kwa wanawake wenye ugonjwa saratani ya shingo ya kizazi”, alisema Dk, Doyin.
Pia kwa kipindi cha miaka mitatu Shirika la Misaada la Marekani (UNAIDS) limetoa dola 33,000 kwa ajili ya kusaidia ushiriki wa wanawake wenye VVU na kufanya kazi na vikundi vidogovidogo katika jamii. Taasisi ya Bristol –Myers Squibb kwa kipindi cha miaka mitatu imetoa dola za kimarekani milioni 1.2 kwa ajili ya kusaidia huduma za kuhamasisha jamii kuhusu vikoba na kuimarisha huduma za jamii
No comments:
Post a Comment