Saturday, 9 November 2013

ST. LAURENT DIABETES CENTRE YAZINDULIWA KUONGEZA JUHUDI ZA KUKOMESHA KISUKARI


IMG_9905Kituo cha Kisukari cha St. Laurent ni kituo cha kisasa cha kupima, kuelimisha na kudhibiti ugonjwa wa
Kisukari. Uzinduzi rasmi wa kituo hiki kitakuwa tarehe 13 mwezi huuwa 11 mwaka 2013. Kwamujibu wa Mkurungezi Mtendaji wa kituo hicho, Dr. Mary Mayige, uzinduzi huo utafanyika kwenye Kituo hicho

kilichopo katika jengo la Msasani Multipurpose Development Trust, mkabala na hospitali ya macho ya
CCBRT. Tafrija ya uzinduzi itafanyika kuanzia saa tisa alasiri mpaka saa kumi jioni (9:00 – 10:00).
Dr. Mayige ameongeza kwakusema kuwa kutakuwa na upimaji wa bure wa Kisukari kwa wote siku ya
jumapili ya tarehe kumi Novemba 2013(10-11-2013) kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni
(2:00 – 10:00), hapohapo kituoni.
Pia, ameongeza kuwa kituo kitatoa elimu ya afya kupitia vipindi vya runinga na makala katika magazeti.
Ameendelea na kusema kwamba elimu ya lishe na maelekezo mengine kuhusu Kisukari yanapatikana
katika ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa facebook ambapo kila mmoja anaweza kupata elimu hasa
vijana.
Kituo cha Kisukari cha St. Laurent kinatoa huduma za kisasa kama nilivyosema awali, kwa wagonjwa
wenye tatizo la Kisukari na shinikizo la damu pamoja na magonjwa ya moyo.
Kituo cha Kisukari cha St. Laurent wanatoa pia huduma za upimaji wa Kisukari, Magonjwa ya Moyo na
wanafundisha jinsi ya kudhibiti na kukabiliana na athari na madhara ya Kisukari kwa wagonjwa wa
Kisukari. Wanapokea wagonjwa wa nje, huduma ya maabara na vipimo vya Kisukari na Magonjwa ya
Moyo. Vile vile, kituo kinatoa ushaurinasaha na elimu ya lishe kamilifu na jinsi ya kudhibiti unene
uliopitiliza. Huduma zinatolewa na madaktari wenye uwezo na utaalam na pia wenye lengo la
kuwawezesha wananchi kuweza kudhibiti na kuzuia kupatwa na magonjwa haya kwa kutoa elimu ya
lishe kamilifu na bora hapo hapo kituoni.
Kituo kinatumia miundombinu bora na ya kisasa katika kutunza taarifa za kila mgonjwa anayefika kituoni
hapo, na wanahakikisha kwamba taarifa zote muhimu zinachukuliwa na kutunza kwa usiri mkubwa na
pia wagonjwa hupewa taarifa ya udhurio lijalo kabla ya tarehe husika ya kumwona Daktari. Huduma
zinatolewa kwa ahadi maalum baina ya mgonjwa na Daktari ili kuhakikisha kuwa wagonjwa wote wana
Page 2
hudumiwa kwa wakati mwafaka bila kupoteza muda wa wagonjwa na kuepuka kupoteza siku nzima kwa
kumwona Daktari.
Dr. Mayige ameendelea kwa kusema yakuwa wameona ni vyema kwa kituo hicho kuwa hapa Dar es
Salaam kwasababu Dar es Salaam kuna ongezeko kubwa la watu wenye matatizo ya shinikizo la damu,
magonjwa ya Moyo na Kisukari na hii imesababisha kuwa na ongezeko kubwa la hitaji la huduma za
kudhibiti na kuzuia magonjwa hayo. Magonjwa haya yanahitaji kituo maalum ili kuweza kutoa huduma
na elimu kwa watu wote wenye matatizo hayo.
Inasemekana kuwa kuna zaidi ya milioni 347 ya watu duniani kote wanaishi na ugonjwa wa Kisukari.
Mwaka wa 2004, watu milioni 3.4 walikuwa na ugonjwa wa Kisukari. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo
vinavyotokana na Kisukari hutokea katika nchi maskini. Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema
kwamba ifikapo mwaka wa 2030, ugonjwa wa Kisukari utakuwa ni sababu ya saba (7) ya vifo duniani.
Katika bara la Afrika, ugonjwa wa Kisukari ni tatizo kubwa na linalokuwa siku baada ya siku. Inafikiriwa
ya kuwa mmomonyoko wa lishe ya kitamaduni na kutokuwa na mazoezi ya mwili ni chanzo kikubwa cha
ongezeko la tatizo hili au ugonjwa huu wa Kisukari.
Kwamujibu wa tafiti zilizotolewa mwaka wa 2000, ongezeko la ugonjwa wa Kisukari linazidi kukuwa
kutoka asilimia moja (1%) katika miaka ya 1980 mpaka kufikia asilimi sita (6%). Inakadiriwa kuwa katika
nchi za Afrika pamoja na Tanzania, ongezeko hili litakuwa zaidi ifikapo mwaka wa 2030. Ongezo la
ugonjwa huu wa Kisukari linamaanisha kuwa asilimia wa watu wenye umri kuanzia umri wa miaka ya 20
mpaka 79 wana Kisukari aina ya kwanza au aina ya pili ya Kisukari. Watu wengi Tanzania wapo katika
hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la Damu kwasababu ya mpangilio mbovu wa
lishe/chakula na kutofanya mazoezi.
Kisukari ni nini?
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha sukari katika damu, na hii inasababishwa
na kongosho kuzalisha kiwango kidogo cha kichocheo cha insulin, au insulin haipeleki sukari
inayohitajika katika seli/chembehai. Sababu zote hizo zinaweza kusababisha Kisukari. Mgonjwa wa
Kisukari hupata matatizo ya kujisaidia haja ndogo marakwamara, hupata kiu kisichoisha na kikali, na pia
mgonjwa huhisi njaa kali marakwamara

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!