Sunday, 24 November 2013

SEKRETARIET KUU YA CCM YAWASILI MJINI MBEYA, IKIWA NA KAULI MBIU YA "UMOJA NI USHINDI"


Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani kati),Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro (kulia) pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia wakazi mbalimbali waliofika kuwalaki mapema leo walipokuwa wakiwasili kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.  
 Pichani shoto ni Nahodha Mkuu wa Meli ya Mv Songea akitoa maelezo mafupi namna ya moja ya chombo cha meli kinavyofanya wakati ikisafiri majini, kwa Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mapema leo walipokuwa wakienda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.Pichani kulia ni Nahodha msaidizi wa Meli ya Mv Songea.Conrad Shauritanga akiongoza meli hiyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!