Monday, 28 October 2013

WAZIRI NCHIMBI ALIPOKWENDA KUMJULIA HALI MZEE ABRAHAM SEPETU ENZI ZA UHAI WAKE


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia), alipokuwa akimjulia hali mzee Isaac Abraham Sepetu Septemba 21, 2013 nyumbani kwake Sinza-Mori, jijini Dar. Ni kama vile alikwenda kumpa mkono wa mwisho wa kwaheri. VIDEO HAPO CHINI INAONYESHA TUKIO HILO:
Baba mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa wa filamu nchini, Wema Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu mapema leo amefariki dunia.
Mzee Sepetu amefariki akiwa katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na Kiharusi alioupata hivi karibuni mjini Zanzibar.
WASIFU MFUPI WA MAREHEMU MZEE  ABRAHAM SEPETU
Mzee Sepetu aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Kati ya mwaka 2001 na 2006 Mzee Sepetu alikuwa Mbunge katika Bunge la Afrika Mashariki.
Pia, Jumatano, Machi 27, mwaka huu, Mzee Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohammed Shein, kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA).

GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!