Saturday, 26 October 2013

TOKA NILIPOANZA KUANDIKA BLOG HII MPAKA SASA HIZI NDIZO HABARI ZILIZONIKWAZA KULIKO ZOTE!

HAWA WAZEE NI WA FAMILIA MOJA WALICHOMWA MOTO KWA KUSHUKIWA KUWA NI WACHAWI.
MASWALI NINAYOJIULIZA NI KWA HAO WALIOSIMAMA PEMBENI WAKISHUHUDIA MATUKIO KAMA HAYA HIVI KWELI HAKUNA HATA MMOJA WAKUWAONEA HURUMA NA KURIPOTI POLISI? MAANA KATIKA HIZI VIDEO ZOTE MBILI WAHUSIKA HAKUNA ALIYEKAMATWA( INASIKITISHA )

HUYU KIJANA ALISINGIZIWA MWIZI, WAKAMUUA SOMA HABARI YAKE HAPO CHINI....

TUNAOMBA RADHI KWA VIDEO HIIJAMANI TANZANIA KUNA NINI? YAANI SITAKI KUAMINI KUWA HII NI TANZANIA HEBU JIONEE MWENYEWE! SINA LA KUSEMA! BODABODA WAUA.....POLISI WAKO WAPI?

Na: Haruni Sanchawa   
Albugas Shiyo, 41, ameuawa kikatili na madereva wa Bajaj na wa pikipiki maarufu kama Bodaboda, baada ya kuitiwa mwizi na dereva wa Bajaj iliyomgonga na kukataa kumpeleka hospitalini.
Tukio hilo lilitokea Chang’ombe Maduka Mawili, Temeke jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wakati marehemu akiwa na wenzake wakitokea katika shughuli zao Kigamboni Wilaya ya Temeke jijini Dar.
Mauaji hayo yamewachanganya wakazi wa eneo hilo ambalo inadaiwa kwa kipindi kirefu hakujawahi kutokea uhalifu na wamefadhaika kwa kuwa aliyeuawa ni mtu ambaye alikuwa anaishi katika eneo hilo kipindi cha nyuma kabla ya kuhamia alikojenga, Majohe, Ilala jijini hapa.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa marehemu ambaye kazi zake zilikuwa ni fundi ujenzi, alikuwa akitoka kazini akiwa na wenzake wawili waliotajwa kwa jina mojamoja;  Zahoro na Baba Mwalimu wakitokea katika ‘saiti’ ya ujenzi Kigamboni.
“Walipofika katika maeneo ya Keko wakiwa wanatembea kwa miguu, Shiyo aligongwa na Bajaj na kuumia mkono wa kushoto, akamuambia dereva aliyemgonga kuwa ampeleke hospitali kwa kuwa amemuumiza,” kilisema chanzo chetu eneo la tukio.
 Inadaiwa kuwa dereva huyo aliyetajwa kwa jina moja la Omary, alikataa kumpeleka hospitali na kukatokea mabishano kati yake, marehemu na wenzake aliokuwa nao ambao waling’ang’ania kwenye Bajaj lakini dereva aligoma.
Hata hivyo, dereva huyo aliamua kuondoka nao hadi katika kituo chake cha kazi, akawageuka na kuanza kupiga yowe kuwa watu hao ni wezi wanataka kumnyang’anya Bajaj yake, ndipo madereva Bodaboda walipojitokeza kwa wingi na kuanza kuwapiga.
“Wenzake walifanikiwa kukimbia lakini yeye kwa kuwa alikuwa tayari majeruhi wa mkono alishindwa, akapigwa hadi akaishiwa nguvu,” alisema shuhuda huku akiomba jina lake kuhifadhiwa.
Alisema baada ya madereva kuona Shiyo ameishiwa nguvu, walianza kumpanda mmoja baada ya mwingine kwa pikipiki zao hadi walipohakikisha amekufa, wakatafuta tairi na petroli kisha wakamchoma moto.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili huku wakiomba majina yao kutoandikwa gazetini kwa kuhofia usalama wao, walisema kuwa kijana aliyemgonga marehemu ni mtu wa matukio na baada ya tukio hilo alikuwa anatamba mtaani kuwa amemfanyizia marehemu na hakuna mtu atakayemfanya kitu.
“Ni kawaida kwa madereva wa Bajaj au pikipiki kuvamia hata madereva wa magari wanapofanya makosa na kujichukulia uamuzi wa hata kulichoma gari wakati pengine makosa wamefanya wao.
“Wengine ni wezi, akina mama wengi wameporwa mabegi yao na hawa madereva wa bodaboda, ingefaa viongozi wa serikali wakavalia njuga hili tatizo,” alisema mtu mmoja.
Daktari mmoja wa Hospitali ya Temeke alisema marehemu aliungua kwa asilimia 90, hali iliyosababisha apoteze maisha.
“Hawa watu walidhamiria kumuua kwa sababu nimeambiwa walimvisha tairi shingoni na kumchoma kama kibaka,” alisema daktari huyo aliyesema asiandikwe jina kwa kuwa siyo msemaji wa hospitali.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Englebert  Kiondo alipohojiwa, alisema: “Tukio hilo lipo na liko katika uchunguzi. Hadi sasa tunamshikilia mtu mmoja  kuhusiana na mauaji hayo.”

2 comments:

Anonymous said...

Good way of describing, and fastidious post to take facts on
the topic of my presentation topic, which i am going to deliver in academy.



My site gender predictor

Anonymous said...

Remarkable things here. I'm very satisfied to look your article.
Thanks so much and I'm taking a look forward to touch
you. Will you please drop me a mail?

My web page gender selection cost (https://www.youtube.com/)

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!