Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameihakikishia kampuni ya China Daliang International Group (CDIG) kwamba serikali inaandaa taratibu za haraka za kuweka dhamana ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 136 upatikane haraka ili ujenzi wa kinu cha kuzalisha umeme uanze mapema mwaka ujao. Pinda ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini hapa kwa mwaliko wa serikali ya China, alisema jana kwamba mradi huo ni muhimu kuanza haraka na kukamilika kwa wakati kwani utakuwa umesaidia kuondoa tatizo la nishati ya umeme nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment