Wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao walipewa jukumu la
kuchunguza kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria wamesema
katika ripoti yao kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuwepo matumizi ya
silaha hizo aina ya sarin katika mauaji ya Agosti 21 karibu na mji wa
Damascus.
Ukurasa wa kwanza wa ripoti, hiyo iliotolewa Jumapili kwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambayo itawasilishwa
kuwasilishwa Jumatatu kwa Baraza la Usalama, na kuongeza kuwa silaha za
kemikali zilitumika kwa kiwango kikubwa wakati wa vita nchini Syria.
Hayo ni wakati mataifa ya Ufaransa, Marekani
na Uingereza yakikutana leo Jumatatu jijini Paris kujadili kuhusu
rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kuweka
sawa makubaliano ya Marekani na Urusi juu ya silaha za kemikali za
Syria wakati wakati ripoti muhimu ya wakaguzi kwa Umoja wa Mataifa
kuhusu mauaji, ya Agosti 21, ikisubiriwa kutolewa.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande akiambatana na
waziri wake wa mambo ya nje Laurent Fabious, wamewapokea mapema leo
asubuhi, mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague na John
Kerry wa Marekani ambao wanajadili kuhusu muswada wa rasimu ambao
viongozi wanatarajia kupasisha kabla ya juma hili kumalizika.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabious
amesema nchi yake itazingatia ripoti ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa
kuhusu mauaji ya Damascus inayotarajiwa kutolewa Jumatatu ili kusitisha
msimamo wake. Ameyasema hayo wakati alipompokea katika katika Ikulu ya
rais ya Quai d'Orsay mwenziye wa Uingereza, na kuungana na waziri wa
mambo ya nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki-moon, ripoti hiyo ya wakaguzi kuhusu matumizi ya silaha za Kemili
itahitimisha matumizi ya silaha hizo bila kutaja muhusika wa mauaji ya
watu 21 Aout yaliosababisha mauaji ya watu elfu moja na mia tano, kwa
mujibu wa Marekani.
Kwa mujibu wa duru za kidiplomasia, serikali ya
Paris inapanga kutumia ripoti hiyo ili kupata uunfgwaji mkono kwenye
Umoja wa Mataifa, ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema
inabidi kuandaa vikwazo iwapo hakutakuwa utekelezwaji wa mkataba na
kwamba kuharibu silaha za kemikali ni hatuwa ya kwanza muhimu, lakini
sio njia ya kufikia suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini Syria.
Ma waziri wa mambo ya nje wa Marekani Johna Kerry
na mwenziwe wa Urusi Sergei Lavrov wameafiki kukutana Septemba 28 ili
kupanga kalenda ya mkutano wa amani kuhusu Syria.
Urusi inaweza kuunga mkono uingiliaji kijeshi
nchini Syria iwapo serikali ya Syria itakiuka makubaliano. Hata hivyo
waziri Lavrov amesema Urusi itafanya uchunguzi kuhusu taarifa zote za
tuhuma dhidi ya serikali ya Syria
No comments:
Post a Comment