Mwanamke mmoja Mjane
aliyefahamika kwa jina la FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU
Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia
pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa na nyoka alipokuwa amelala chumbani
kwake.
Mjane huyo alijeruhiwa
mkono wa kushoto na nyoka alipokuwa amelala chumbani kwake hivi karibuni na
kusababisha ngozi kutoka hali iliyomsababishia maumivu makali ambapo alikimbizwa
Hospitali ya Wilaya ya CHUNYA na kupatiwa matibabu lakini mpaka sasa hali
inazidi kuwa mbaya.
FAINES amesema pamoja na kupatiwa matibabu katika
Hospitali ya Wilaya na kuruhusiwa kurudi nyumbani mkono umezidi kuliwa na sumu
na kusababisha ngozi kutoka hadi mfupa kutokeza nje ya ngozi hali inayomtia hofu
siku hadi siku.
Mama huyo hana pesa za
kuweza kupata matibabu zaidi kutokana nayeye kufiwa na mumewe na wanawe hawana
uwezo wa kugharamia matibabu katika Hospitali nyingine hivyo kuwaomba wasamaria
wema kumsaidia ili aweze kuokoa maisha.
Baadhi ya majirani
wamesema mama huyo ameumwa na nyoka siku za hivi karibuni akiwa amelala chumbani
kwake na alipopelekwa kupatiwa matibabu hajapata ahueni na afya yake imezidi
kuzorota siku hadi siku hali akishindwa kufanya kufanya shughuli za
kiuchumi
Picha na Ezekiel
Kamanga
wa
Mbeya yetu
Kwa atakae guswa
kumsaidia mjane huyu wasiliana
na
0754 49 07
52
AU
0754 37 44
08
|
No comments:
Post a Comment