Wednesday 4 September 2013

ARIEL CASTRO AJINYONGA JELA.



index

Maafisa wa magereza katika jimbo la Ohio nchini Marekani wanasema mtu aliyeshikilia na kuwafunga wanawake watatu kwa zaidi ya muongo mmoja amekutwa amekufa.
Ariel Castro alikutwa akinining’inia kwenye jela yake Jumanne usiku. Maafisa wanasema Castro mwenye aliyekuwa na umri wa miaka 53 alipelekwa kwenye hospitali ya karibu na walithibitisha kifo chake.
Dereva huyo wa zamani wa basi la shule alikamatwa mwezi Mei baada ya mmoja wa wanawake aliokuwa akiwashikilia kifungoni nyumbani kwake kutoroka na kukimbilia kwa majirani kuomba msaada.Maafisa wanasema aliteka wanawake hao kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2002 na 2004 na kuwabaka mara kadhaa wakiwa kifungoni.
Chanzo: voaswahili.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!