Wednesday 7 August 2013

TAARIFA YA SIKUKUU YA EID KUTOKA POLISI.

Advera-SensoJeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.
Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.
Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, wanatakiwa kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!