Saturday, 13 July 2013

"WAPINZANI BADO NI WACHANGA SANA KUWARUHUSU WAINGIE IKULU"... MKAPA



RAIS mstaafu, Benjamin William Mkapa, ameonyesha wazi kutoridhishwa na mwenendo wa matukio ya uvunjifu wa amani hivi sasa. 


Mkapa, mmoja wa viongozi ambao wanajiamini katika kauli zao, amewataka Watanzania kutochoka kusali na kuiombea nchi ili amani iendelee kutawala. Alisema jukumu hilo linawahusisha watu, wakiwamo viongozi wa dini ambao wana dhamana kubwa kwa waumini wao.

Mkapa alitoa kuali hiyo jana mjini Mwanza, muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi, katika jengo la ghorofa nne la Chuo Kikuu cha Sayansi, Tiba na Afya, kinachomilikiwa na Hospitali ya Bugando. “Watanzania tukitaka uchumi wetu ukue, lazima nchi iwe na amani, bila hali hiyo hakuna chochote kitakachofanyika.
 

"Ndugu zangu, nawaomba Watanzania wote kwa itikadi zao, tuwaombee viongozi wetu wa dini ili wawe na ushirikiano mzuri...na wao waliombee taifa hili, hii ni tunu tuliyopewa,” alisema Mkapa.


Alisema yeye anatambua Mungu alimpangia kuongoza Watanzania, jambo ambalo lilitimia kwa kipindi cha miaka 10 ya kuliongoza taifa.

Habari zaidi zinasema, jana jioni alitarajiwa kuongoza harambee ya kukusanya Sh milioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la Chuo Kikuu cha Sayansi, Tiba na Afya, ambayo itahudhuriwa na watu mbalimbali.


Juzi, Rais Jakaya Kikwete wakati akifunga kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), alikiri kuwapo na viashiria vya uvunjifu wa amani nchini.

Alisema katika siku za karibuni, kumeibuka viashiria vingi, vikiwamo vya watu kutangaza kuanzisha vikundi vya mgambo kwa ajili ya kujilinda.


CCM
Katika hatua nyingine, Mkapa aliwasihi vijana kudumisha amani na mshikamano uliopo


Aliwapongeza na kuwataka kuendeleza mshikamano na umoja ndani ya chama ili vijana wasipotoshwe na wasiasa wanaotaka madaraka kwa hila na kuleta machafuko nchini kwa lengo la wao kukimbilia Ikulu kushika madaraka makubwa ya nchi, wakati bado wachanga.

Mkapa alimwagia Mbunge wa Bariadi Magharibi,John Cheyo (UDP) kutokana na kauli aliyoitoa kwenye semina ya kongamano la amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), aliposema kikosi kipya kinachotaka uongozi wa Taifa hili kina wajibu wa kujifunza.

Mkapa akinukuu maneno ya Cheyo, alisema “kikosi kipya kinachotaka madaraka hakielewi na hakitaki kukili kwamba taifa hili na nchi hii inahistoria, mira na tunu zake za kutawala .

“Kwa kweli tusiombee wapinzani hawa washike nchi hawafai na haifanani kabisa na kauli, lugha na matendo yao,wanadhani wakishika madaraka makubwa ya nchi hii itasitawi zaidi kuliko ilivyo kwa CCM? Si kweli hata kijiji hawajaweza kutawala na hata hivyo wanavyotawala na majimbo hali yake ni ya hovyo”alisema

“Kizazi kipya hakitaki kukiri na kutambua kama nchi hii ina historia, mira, desturi zake na hata tunu za kutawala, ni vyema wakalitambua na kujifunza badala ya kuanza kuivuruga amani, umoja na utulivu kwa lengo la kukimbilia kushika madaraka makubwa
 
CHANZO MPEKUZI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!