Monday 22 July 2013

WAASI WA M23 WAKIELEZEA JINSI WALIVYOMTEKA MWANAJESHI WA TANZANIA

 







Waasi hao wa M23 wameweka  picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter. Kwa mujibu wa chimpreports.com, M23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Ifuatayo ni kauli ya M23 waliyoweka Facebook ikiambatana na picha hiyo: “leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe. Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!