Na Mwandishi Maalum
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumatatu lilikuwa na majadiliano juu ya kukosekana kwa usawa wa kiuchumi na kijamii kati ya mtu na mtu, na baina ya nchi na nchi na adhari zake kwa mstakabali wa amani, usalama na maendeleo endelevu.
Majadiliano hayo ya siku moja yaliandaliwa na Rais wa Baraza Kuu Bw Vuk Jeremic na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, yaliwahusisha baadhi ya mawaziri kutoka nchi kadhaa, wakuu wa Mashirika yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa, Jumuiya za Kikanda pamoja na Asasi zisizo za kiserikali.
Akifungua majadiliano hayo, Katibu Mkuu amesema, licha ya kuwapo kwa mafanikio kadhaa katika upatikanaji wa huduma za kijamii, kama vile afya, elimu, maji safi na salama kupitia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs). Bado pengo kati ya walionacho na wasio nacho ni kubwa na linaendelea kukua.
Kwa mfano, anasema, katika miaka michache iliyopita jumuiya ya kimataifa imeshuhudia ongezeko la idadi ya watoto wanaokwenda shule hasa watoto wa kike, kupungua kwa vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga, na vita dhidi ya magonjwa kama vile malaria, maambukizi ya ukimwi na kifua kikuu.
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI














No comments:
Post a Comment