Monday 17 June 2013

WACHIMBA MCHANGA WAVAMIA MAKABURI NA KUSAMBARATISHA MIILI YA WANANCHI WALIOKUFA NA KUZIKWA ILALA!!!

WAVAMIA MAKABURI NA KUSAMBARATISHA MIILI YA WANANCHI WALIOKUFA NA KUZIKWA ILALA!!!




Wachimbaji mchanga wakiendelea na shughuli zao pamoja na malalamiko ya wananchi wa Kata ya Msongora kuhusiana na kufukuliwa makaburi na kusababisha barabara inayounganisha Kata ya Chaninika na Kivule kuharibika. 

  • Wameanza kuchimba eneo hilo kwa zaidi ya mwezi sasa baada ya kuruhusiwa na mwenye eneo hilo wakitafuta fedha za kutunza familia zao kama wengine.
Ni wachimba mchanga ambao wanadai wamepewa ruhusa na mwenye eneo linalodaiwa kuwa makaburi awai.
Dar es Salaam. Watu wasiojulikana, wamevamia eneo la makaburi na kuanza kuchimba mchanga na kusababisha baadhi ya viungo vya binadamu kubakia juu katika makaburi ya eneo la Kurutini Kata ya Msongora Manispaa ya Ilala.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya watu hao wasiojulikana kuvamia eneo hilo na kuanza kuchimba mchanga jambo lililosababisha mabaki ya miili ya watu kufukuliwa na kuwekwa pembeni huku wavamizi hao wakiendelea na uchimbaji wa mchanga huo.

Akizungumza jana Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mbondole,Amos Sibola alisema, baada ya kupelekewa malalamiko na wananchi wa mtaa huo, walilazimika kufika kwenye eneo hilo na kukuta uchimbaji huo ukiendelea huku makaburi yakiwa yamefukuliwa.
Sibola alisema aliwafuata wapakizi na wenye magari yanayopakiwa mchanga huo na walimjibu kuwa walipewa kibali na mwenyeji wa eneo hilo la makaburi ambaye aliwaruhusu kuchimba mchanga huo.
“Wakati tunaongea mpakizi mmoja akiwa anachukua  mchanga ili aweke kwenye gari alirusha kiungo cha mkono ambapo ulichukuliwa na kufukiwa eneo lingine huku wakiendelea na uchimbaji huo,” alisema Sibola.

Sibola alisema, baada ya kutokea uharibifu huo walimwandikia barua Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Mei 16, mwaka huu kuhusiana na machimbo ambayo sio rasmi lakini hakuna hatua iliyochukuliwa huku uchimbaji huo ukiendelea sehemu mbalimbali kwenye kata hiyo.


Pia alisema barabara kuu ya kata hiyo inayounganisha kata mbili ya Kivule na Chanika imeharibiwa kutokana na machimbo hayo.
Alisema wavamizi hao wamechimba mchanga huo na kuharibu barabara ya Shule ya Sekondari ya Holy Familiy hivyo mvua zitakapoanza kunyesha barabara hiyo haitapitika. Mpakizi Hassan Abdallah alisema wameanza kuchimba eneo hilo kwa zaidi ya mwezi sasa baada ya kuruhusiwa na mwenye eneo hilo wakitafuta fedha za kutunza familia zao kama wengine.
 
 
 
 Picha na Pamela Chologola

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!