Zitto Kabwe amefunguka na kudai kuwa kwa sasa
wanajiandaa kufanya mapinduzi
ya nchi endapo serikali watu walioficha mabilioni uswiswi
hawatashughulikiwa ipasavyo....
Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya
fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo
200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo
inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari
imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la
Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi
huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho
cha Bunge.
Zitto Kabwe anatoa
angalizo katika hatua hiyo ya jaji Werema kwa kusema kuwa hatua hii
isiwe "zima moto" na daganya toto ili kuwafumba macho
watanzania...
Ubabaishaji wowote kwa mujibu wa Zitto Kabwe utasababisha mapinduzi ya nchi.....
Hii ni post yake aliyoweka katika mtandao wa twitter
Habari kwa hisani ya Mpekuzi.
No comments:
Post a Comment