Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika.
Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40.
Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic.
Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya haiathiriki na tukio hilo.
Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj.
Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi tangu alipopokelewa hospitalini hapo.
Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika
Kusini mwaka 1994, alikimbizwa hospitali moja ya Pretoria mapema Juni 8 kufuatia
maambukizi kwenye mapafu.
Ilidaiwa jana kwamba Mandela
hajitingishi na familia yake sasa inajadili uwezekano wa kusitisha
matibabu.
Amekuwa hospitalini kwa wiki mbili akipambana na
maambukizi hayo, lakini taarifa zilizopita zimeashiria kwamba afya ya Mandela
inaimarika.
Kwa mujibu wa vyanzo vipya, ufanyaji kazi wa ini na figo za Mandela umeshuka kwa asilimia 50 na hajaweza kufungua macho kwa siku kadhaa.
Historia ya matatizo ya mapafu ya Mandela ilianzia
tangu alipokuwa kwenye gereza la Kisiwa cha Robben karibu na Cape Town.
Aliachiwa huru mwaka 1990 baada ya miaka 27 na akaendelea kutumikia nchi kama
Rais kuanzia mwaka 1994 hadi 1999.
Kulazwa kwake hospitalini ni mara ya nne tangu Desemba,
mwaka jana.
SOURCE MPEKUZI.
No comments:
Post a Comment