
Kikosi cha timu ya Taifa Taifa Stars
************************************************************
Taifa Stars inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia kwa kesho (Juni 8 mwaka huu) kuikabili Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade hapa Marrakech, Morocco.
Ilipoteza ya kwanza ugenini dhidi ya Ivory Coast mwaka jana, na kushinda mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco. Mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Morocco ni ya pili kwa Stars katika uwanja huo ambapo mwaka juzi ilifungwa mabao 3-1.
Washabiki wa Morocco wanaonekana kuikatia tama timu yao yenye pointi mbili tu nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kundi hilo la C ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Tanzania yenye sita. Huo ni mtazamo wa washabiki, lakini kwa upande wa timu inaonekana imepania kujichomoa katika nafasi za chini
Kwa upande wa Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake imepania mechi hiyo, lengo likiwa ni kuona inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mechi hiyo itakayokuwa chini ya refa Daniel Frazier Bennett wa Afrika Kusini.
Amesema timu yake itacheza kwa umakini na uangalifu kwa vile wanajua wapinzani wao wakicheza mbele ya washabiki wao watakuwa katika shinikizo za kushinda, jambo ambalo wamejiandaa kukabiliana nalo.













No comments:
Post a Comment