skip to main |
skip to sidebar
STEVEN KANUMBA JR AZALIWA, MAMA KANUMBA, MAMA LULU NA LULU WAJAWA NA FURAHA. !
Mama Lulu na mama wa
marehemu Steven Kanumba wanaonekana kuwa karibu sana siku hizi na hivyo watu
kuzidi kuamini kuwa hawana tofauti tena na kusahau yaliyopita. Dada wa marehemu
Steven Kanumba amejifungua hivi karibuni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
na mtoto huyo kupewa jina la Steven Kanumba Jr huku mama mzazi wa Elizabeth
Michael(Lulu) na mama Kanumba wakiwa na furaha sana, Lulu pia alionyesha furaha
yake kwa kuzaliwa mtoto huyo kama picha zinavyoonekana hapo juu. Tunawapongeza
tena na tena wazazi hao kwa kuwadhihirishia wanajamii kwa mara nyingine kuwa
kila mtu ana amani na mwenzake na hakuna tofauti yoyote kati yao. Mtoto huyo
amepewa jina la Kanumba kama ishara ya kumuenzi muigizaji Steven Kanumba
aliyekuwa maarufu Afrika mashariki na kuanza kujulikana kimataifa.
No comments:
Post a Comment