Tuesday, 25 June 2013

MTANGAZAJI WA EATV JOYCE KIRIA AMTAFUTA MUMEWE KWA MABANGO, AOMBA RAIS AINGILIE KATI, HAJUI MUMEWE ALIPO.



Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake katika Television ya EATV, Bi Joyce Kiria, akiwa nje ya jengo la Habari (maelezo) Mtaa wa samora, mara baada ya kuzungumza na waandishi wa Habari kuhusu, Mume wake Bw Henri Kileo, ambaye inasemekana kwamba anashikiliwa na jeshi la Polisi, na kwamba mwanamama huyo hajaambiwa chochote wapi alipo mume wake, na nini kinaendelea juu ya mkasa huo. akiongea kwa sauti Joyce amemuomba Mheshimiwa Rais na wananchi kwa ujumla wamsaidie.
Kwa upande wa Polisi walitoa maelezo haya.
Advera-Senso Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!