Monday, 24 June 2013
: MSANII WA WAKO 2 NAKO AACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA, AJIUNGA NA TAASISI KWA MATIBABU .
Kupitia sammisago.com Rapper Ibra Da Hustler amefunguka kuwa sasa anampango wa kubadilisha maisha yake na jambo alilo anza nalo ni kuachana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya Herion na Crack Cocaine. Da Hustler ameniambia kwenye exclusive interview niliyo mfanyia kuwa.
1] Nimeacha Kabisa madawa na nina siku nne sijagusa toka nimejiunga na hii taasisi, nimejifunza kuvumilia arosto na matumaini yangu ni kuacha kabisa madawa kwani yameharibu maisha yangu kabisa. Ni Uharibifu wa pesa nyingi na umekaribisha dharau kwenye maisha yangu
2] Nikifanikiwa kuwa sober kabisa mpango wangu ni kurudi vizuri kwenye mziki kwani ndio uwezo wa kazi nilionao na najua mashabiki bado wana hamu na kazi zangu.
3] Nako 2 Nako na Weusi wananipa ushirikiano mzuri sana, wote wamefurahi kusikia nimeacha madawa na Lord ndio aliye nipigia simu kuniambia nimefanya jambo msingi.
4] Yes ni kweli kuna binti alini shawishi kutumia madawa na ndio najutankumfahamu na kwanini nilikubali. Nimegundua hataki maendeleo yangu kabisa nanimejifunza kutoka kwake, sasa nikimuambia mtu usiguse madawa ataamini kwani najua kitu gani atapata kwenye maisha yake.
5] Wimbo Wa Sababu Ni Wewe Nimeimba mambo yote yaliyo nitokea toka nimeanza kutumia madawa na jinsi yalivyo mess up my life, Matumaini yangu vijana watajifunza kutoka kwangu kuhusu madhara ya hii kitu.
SOURCE Sammisago.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment