Monday 17 June 2013

MAMA AIBIWA MTOTO MCHANGA, MARA BAADA YA KUJIFUNGUA HUKO SHINYANGA.

Mama aibiwa mtoto mchanga akiwa wodini




Neema Sawaka,
MWANAMKE mmoja Modesta Sumbuko (26) (pichani) anadaiwa kuibiwa mtoto mchanga wa kiume katika chumba cha upasuaji alipokuwa akijifungua na watu wasiojulikana katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Sumbuko ambaye ni mkazi wa kijiji cha Butende kata ya Mpunze Wilayani hapa alidai kuibiwa mtoto wake wa kiume wa siku tatu katika hospitali hiyo akiwa ndani ya wodi ya wazazi alikokuwa amelazwa baada ya kujifungua kwa njia ya operesheni.
Akielezea mkasa huo akiwa katika kitanda chake kwenye wodi ya wazazi, Sumbuko alidai kuwa mwanaye aliibiwa saa 11 alfajiri wakati akiwa amelala na kwamba baada ya kuamka aliangalia na kukuta mtoto hayupo.
Wakielezea tukio hilo wanawake waliokuwa katika wodi hiyo walidai kumwona mwanamke mmoja ambaye aliingia wodini akiwa amevaa hijabu na ushungi akielekea katika kitanda cha mwanamke huyo.
Mume wa mama huyo Emmanuel Matheo alidai kuwa mke wake alimleta katika hospitali hiyo jumatatu ili ajifungue ambapo kutokana na matatizo alizaa kwa njia ya kufanyiwa upasuaji.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dk Andrew Emmanuel alikiri na kuthibitisha kuibiwa kwa mtoto huyo katika wodi ya wazazi alikokuwa amelazwa Sumbuka baada ya kujifungua.
 
 
habari kwa hisani ya Neema Sawaka.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!