![](https://fbcdn-sphotos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash4/420849_321919571179054_104017002_n.jpg)
KIPA wa Simba, Juma Kaseja, amesema kwa sasa hawezi kujiunga
mapema katika mazoezi ya kikosi hicho kutokana na kwamba hana
mkataba na klabu yoyote.Kauli hiyo ya Kaseja inakuja kufuatia kipa huyo mkongwe
kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, ambao ulifikia
tamati mwishoni mwa msimu uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano,
Kaseja alisema kwa sasa
hawezi kujiunga mapema na kikosi hicho alichokitumikia
hadi msimu uliopita kwa kuwa hana mkataba na timu hiyo
baada ya ule wa awali kumalizika.
Kaseja alisema kwa sasa atakuwa na mapumziko ya siku chache
baada ya kumaliza majukumu ya Taifa Stars, ambapo atajua
hatima ya timu atakayoichezea msimu ujao ndani ya siku saba kuanzia juzi.
“Ukiniuliza nitajiunga lini katika mazoezi ya Simba, sidhani kama
nitakupa jibu zaidi ya sijui, kutokana na sasa sina mkataba wowote na
Simba, mimi sasa ni mchezaji huru, mkataba wangu na Simba
ulishakwisha,” alisema Kaseja huku akiongeza kwa kusema:
“Hivi ninavyoongea na wewe (juzi jioni), ndiyo kwanza hata
nyumbani kwangu sijafika, natoka katika kambi ya timu ya taifa,
nataka kwanza nikapumzike kwa siku kadhaa na baada ya hapo
nadhani ndani ya siku saba nitajua nini nifanye na wapi nitasaini.”
Club itakayonitaka ntakuwa tayari kuzungumza nao kwa
kuwa sina mkataba na simba
umeisha tayari,ni hayo tu nayoweza kuongea kwa sasa

No comments:
Post a Comment