Wednesday, 26 June 2013

TANGAZO . USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZOTE MWISHO JULAI 10. KILA NAMBA YA SIMU LAZIMA IWE IMESAJILIWA.

 


 

Kama ambavyo tayari ilitangazwa awali, siku ya Jumatano, tarehe 10 mwezi Julai mwaka huu namba zote za simu (SIM cards) ambazo hazijasajiliwa zitakuwa si halali kuendelea kutumika na zitasitishwa matumizi yake.

Zoezi la kusajili namba za simu ambalo linaendelea bado halijafanyika kikamilifu kwani zipo namba nyingi zinazotumika ambazo bado hazijasajiliwa na pia uwepo wa watu wengi kutumia majina na vitambulisho bandia kwenye usajili. Baadhi ya mawakala wa usajili wamekuwa wakichangia uwepo wa tatizo hili kwa kutohitaji vitambulisho stahiki toka kwa wanaoomba kusajiliwa.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inashirikiana na Jeshi la Polisi na Mamlaka nyingine za sheria kuwawajibisha wale wote wanaokiuka sheria za usajili na matumizi sahihi ya simu.

HAKIKISHA LINE YAKO YA SIMU (SIMU CARD) IMESAJILIWA KABLA YA SIKU YA JUMATANO

January Y. Makamba

TAREHE 10 MWEZI JULAI, 2013


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!