![](https://fbcdn-sphotos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn1/155222_183912751624865_3737857_n.jpg)
TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’
imechoropoka zimevuja....
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa
jina la wifi 10 cha jijini Dar hivi sasa hana ujauzito tena kama wengi
wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo
fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala
kesho,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana
kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa
siku za nyuma.
Baada ya kupata habari hizo, mwandishig wetu
alilimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Mwandishi: Mambo vipi, Penny
pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Penny: Pole ya nini sasa?
Mwandishi: Si nimesikia
kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo
unaousema maana mimi niko fiti tu.
Mwandishi: Nilisikia kwamba
baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika
3) Asante ni mipango ya Mungu.
Mwandishi: Sasa unatarajia
lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu
ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.
Credit: GPL
No comments:
Post a Comment