Monday 6 May 2013

WATU SITA WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA BOMU LILILOLIPUKA JANA HUKO ARUSHA, AMBAPO IMEELEZWA KUWA WANNE NI RAIA WA SAUDI ARABIA, NA WATANZANIA WAWILI.



DSCN2227

 Vyombo vinavyohusika vimewakama watu sita, ikiwemo raia
 wanne wa Saudi Arabia, kwa kuhusika na shambulizi la bomu lililoua watu watatu na kujeruhi makumi katika kanisa Katoliki la Olasiti, Arusha
Raisi Jakaya Kikwete ameliita tendo hilo kuwa ni la kigaidi..na kwamba wahusika lazima wachukuliwe hatua kali...
 
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amethibitisha
kuwa watu sita wamekamatwa, ambapo kati yao wawili ni Watanzania, na Wanne ni Wasaudi

“Uchunguzi bado unaendelea,” alisema RC Mulongo, na kuongeza kuwa Wasaudi hao waliwasili Arusha Airport siku ya Jumamosi.
 
 
Aliongeza kuwa Watanzania wawili waliokamatwa ni Wakristo. Hakutoa maelezo zaidi


Mlipuko ulitokea nje ya kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Arusha jana tarehe 6.
 
 
Imetafsiriwa kutoka Al-Jazeera

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!