Tuesday 7 May 2013

SERIKALI. SH BILION 876.3 KUTATUA TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI DAR-ES-SALAAM

Gianttrafficjam
Na Immaculate Makilika- Maelezo
SERIKALI imesema   inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336   katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Salender . Alisema   kuwa  inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni  kama ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh.  bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).


Nyingine ni  Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh.  bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh.  bilioni 35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa  msaada wa fedha kwa  ajili ya ujenzi.
 Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya  Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!