Tuesday, 27 July 2021

Mwakinyo No 1 Afrika

 Box Rec imemtaja Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo namba moja kwa bara zima la Afrika na namba 37 Duniani kati ya Mabondia 2,050 kwenye uzani wa Super Welter.

Baada ya taarifa hii Mwakinyo amezungumza na AyoTV na kusema ——— “Namshukuru Mungu na Support ya Watanzania wote na Menejimenti yangu, nimefurahi kwakuwa ni sehemu ya kuona kwamba nipo njiani kutimiza ndoto au safari ninayoiwaza kutokana na vikubwa vinavyozidi kutokea, naamini kupanda kwa rank huku kuna vichocheo vingi zikiwemo Dua za wote wanaonitakia kheri”
“Imekuwa sehemu ya faraja kwangu naamini kuwa namba moja Afrika sio kitu kidogo, sio kila Bondia anaweza kufika na pia sio sifa ya mimi kufika ila naamini ni wakati ambao Mungu ametaka nifike kutokana na jitihada na nguvu nilizowekeza katika kazi yangu” ——— Mwakinyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!