Friday, 23 July 2021

KCMC yakabiliwa na uhaba wa mitungi ya gesi

 


Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Profesa Gilleard Masenga amesema mgonjwa mmoja wa #COVID19 anatumia hadi mitungi 10 kwa siku.

Hospitali ya Rufaa ya KCMC inzalisha mitungi 400 na idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka hali inayofanya hospitali kuzidiwa.


----
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC imezidiwa na idadi ya wagonjwa wanaohitaji hewa ya Oksijeni ukilinganisha na mitungi 400 inayozalishwa kwa siku huku mgonjwa mmoja akitumia mitungi 8 hadi 10 kwa siku.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Julai 23 na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali hiyo, Profesa Gilleard Masenga wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Profesa Masenga amesema kwa siku inatumika mitungi ya Oksijeni zaidi 400 ukilinganisha na uzalishaji wake kwa siku ambayo ina uwezo wa kuzalisha mitungi 400.

"Kwa siku mgonjwa mmoja anatumia mitungi 8 hadi 10 hili tatizo ni kubwa na wananchi msilichukulie kimzaha mzaha ni ugonjwa hatari sana, tuendelee kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya," amesema Profesa Masenga na kuongeza,

"Tuna kiwanda hapa KCMC cha kuzalisha mitungi 400 kwa saa 24 na mtambo huu Mungu alitusaidia tukauweka mwaka jana na tuliona hili litatusaidia kwa miaka 20 bila kuwa na shida ya Oksijeni,"

"Matumizi yetu kwa siku yalikuwa ni mitungi 50 hadi 60 lakini ilipofika mwezi wa tatu mwaka jana kwenye wimbi la kwanza la corona tuliona umuhimu wake,"amesema Profesa Masenga.

"Sasa hivi kiwanda kimezidiwa matumizi ni zaidi ya mitungi 400 kwa siku kwa hiyo hali sio nzuri," amesema Profesa Masenga

Amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo wa corona na kufuata maelekezo yote yanayoendelea kutolewa na Wizara ya afya.

Chanzo: Mwananchi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!