Waliumiza Vichwa Kwa Ajili Yetu...
Hivyo basi, UNIP. Vyama vya ukombozi wa watu wanyonge, Tanzania na Zambia.
Pichani:
Julius Kambarage Nyerere akiwa kwenye mkutano wa PAFMECSA uliofanyika Mbeya katika eneo ambalo sasa pana ukumbi wa Mkapa Hall (Maarufu Soko Matola).
Ilikuwa ni mkutano wa maandalizi ya kuunda OAU. Ni mwaka 1963. Picha inaeleza mengi sana.
Kuna unyenyekevu mkubwa umetawala. Kwamba pamoja na kuwa Zambia ilikuwa haijawa huru, Julius na Rashid walimpa heshima Rais wa UNIP, chama cha kupigania Uhuru wa wa Northern Rhodesia ( Sasa Zambia), kukaa katikati.
Picha inawaonyesha wote wakiwa wamezama kwenye fikra. Hapo hakuna aliyefikiria mambo ya ufisadi kama vile kujipatia utajiri wake mwenyewe. Waliumiza vichwa kwa ajili ya Afrika.
Julius ni kama aliamka na kukumbuka kuvaa sweta kwa baridi ya Mbeya, kitana yawezekana alikisahau!
Rashid Kawawa pamoja na kuangalia mbele, picha inaonyesha kuwa yuko mbali kifikra. Rashid yeye alikumbuka suti yake, na nywele zake za afro zilikolea chanuo.
Naam, jamaa alikuwa 'Handsome boy', katika wakati wake!
Hii ni moja ya picha bora za wakati huo.
Maggid.
No comments:
Post a Comment