Wednesday, 16 June 2021

Mbaroni kwa tuhuma za Mauaji

Dar Es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Shadrack Kapanga mwenye umri wa miaka 34 kwa tuhuma za mauaji ya mama na watoto wake wawili.


Kapanga ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani alikamatwa Juni 11, 2021 eneo la Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya kuwaua Emilly Mutaboyerwa ambaye ni mama na Damita (13) na Daniela Mutaboyerwa (15).
Mtuhumiwa huyo alitekeleza mauaji hayo nyumbani kwa marehemu Masaki Dar es Salaam
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba baada ya kufanya tukio hilo.
“Vitu alivyokutwa navyo wakati akitoroka ni simu za marehemu, televisheni, king’amuzi cha DSTV na rimoti,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Muliro ameeleza kuwa upelelezi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la mauaji Juni 9, 2021 baada ya kuwapiga kila mmoja kwa wakati tofauti kwa kitu kizito na kuwasababishia kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.
Baada ya kuwaua aliwafungia ndani na kutoroka.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!