Friday, 4 June 2021

Kim Kardashian-Mimi ni fungu la kukosa!

 
Mwanamitindo na mtangazaji wa TV nchini Marekani, Kim Kardashian hajafurahia kuachana na Kanye West, kwani amesema anajiona kama yeye ni fungu la kukosa mara baada ya ndoa yake na Rapper Kanye West ikiwa ni ya tatu kuvunjika.

Mtangazaji huyo akiwa kwenye show yake ya ‘Keeping Up With Kardashian’ wakati wa mazungumzo na wadogo zake, alijikuta akiwaliza kwenye episode hiyo mpya huku akitokwa machozi Kim aliendelea kusema Kanye anapaswa "kuwa na mke anayeunga mkono kila hatua yake."
Ikumbukwe mwaka 2000 Kim Kardashian alifunga ndoa ya kwanza na mtayarishaji wa muziki Damon Thomas (Harvey Mason Jr) ilidumu miaka 4 tu, kisha mwaka 2011 akafunga ndoa na mchezaji wa mpira wa kikapu Kris Humphries na kuvunjika 2013, na mwaka mmoja baadaye (2014) akaolewa na Rapper Kanye ambayo pia haikudumu kwani mwaka huu ndoa yao ilifika mwisho.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!