Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu ametangaza ajira za walimu 6,949 wa shule za msingi na sekondari pamoja na watumishi wa Afya 2,726
Nafasi hizi ni kujaza nafasi wazi kutokana na vifo, kustaafu, kuacha kazi au kuhamia sekta nyingine. Waombaji wanatakiwa kuomba kupitia tovuti ya tamisemi, ajira.tamisemi.go.tz kuanzia leo tarehe 9-23 mei, 2021
Maelekezo.
- Maombi ya ajira za UALIMU , yamefunguliwa kuanzia tarehe 2021-05-09 hadi tarehe 2021-05-23
- Maombi ya ajira za AFYA, yamefunguliwa kuanzia tarehe 2021-05-09 hadi tarehe 2021-05-23
- Kama ni muombaji mpya bofya kiunganishi cha juu kulia "Jisajili" kuanza kuomba
- Ingiza namba ya kidato cha Nne ikiwa na mwaka wa kuhitimu kama jina la mtumiaji na uingize nywila yako kuingia ndani ya mfumo.
- Baada ya kufanikiwa kuingia ndani, tafadhali kamilisha maombi yako kabla ya tarehe ya mwisho
- Maombi yasiyokamilika hayatafanyiwa kazi
- Hakikisha kabla ya kutuma maombi umesoma na kuelewa vizuri tangazo lilotolewa
- Bofya hapa ili ujisajili kwa ajili ya kutuma maombi
No comments:
Post a Comment