Ukweli ni kwamba unasikia maumivu tena sanaa ila unayakubali na kuyaelewa.Na zaidi ukiwa katika UTULIVU wa akili na nafsi.Kama hauna utulivu wa nafsi na akili ndugu yangu utatapatapa sanaa mwisho uonekane kichekesho.Utaongea vitu vya ajabu na pengine kufanya vitu vya ajabu.
Sikia maumivu yako
Yakubali maumivu yako
Yaelewe na ujue hakuna unachoweza kufanya kubadilisha.....kama Kipo cha kubadilisha badilisha.
Kuwa mtulivu utavuka tu.
Kama kuna somo la kujifunza katika changamoto hiyo tulia kwani upo darasani na hakikisha unafaulu mtihani huo.
Nakukumbusha tena KUWA MTULIVU....good morning!
Dina Marios
No comments:
Post a Comment