Sunday 4 April 2021

Fundi afa kwa shoti akichomelea

Mkazi wa Mtaa wa Kazaroho, Kata ya Mbugani katika Manispaa ya Tabora, Salumu Madinda amepoteza maisha papo hapo baada ya kupigwa na shoti  ya umeme wakati akichomelea sehemu iliyopasuka kwenye bodi la gari kwa kutumia mtambo wa kuchomelea (welding machine).


Baadhi ya watoto wa marehemu ambao walikuwa naye katika kiwanda chake kidogo cha uchomeleaji muda mfupi kabla ya kupatwa na umauti wake wameeleza namna tukio lilivyo tokea

 wakati baba yao akiwa kazini.

 

"Mzee amefariki kutokana na shoti ya umeme chanzo kikubwa ni kuvuja kwa mashine, ilikuwa inavujisha voltage kwa wingi zaidi lakini zile waya mbili zakuchomea zilikuwa zimelala kwenye ardhi ambayo ilikuwa mbichi na ina unyevunyevu," amesema Juma Salumu, mtoto wa marehemu.

"Mzee alikuwa akichomolea gari aina ya Canter alikuwa amevaa viatu virefu kwa ajili ya usalama wa shoti ya umeme kama kawaida inavyotakiwa lakini kwa bahati mbaya ule unyevu wa chini ya radhi alipopiga magoti ndipo shoti ilipompiga na kupelekea umauti wake," amesema Said Salumu, mtoto wa marehemu.

Muda mfupi baada ya mazishi  kufanyika akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo, Rabani Daudi amesema Jeshi la Polisi lilifika na kujiridhisha juu ya tukio hilo na kuto ruksa ya mwili huo kuzikwa huku akiwaasa mafundi umeme na wananchi wote kuchua tahadhari kazini.
 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!