Watu sita wamefariki papo hapo katika ajali iliyohusisha Basi la Machame lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Arusha katika eneo la Kiongozi Wilayani Babati Mkoani Manyara.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema waliofariki ni wanaume wanne na wanawake wawili ambao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Babati ya Mrara mkoani humo.
No comments:
Post a Comment