Friday, 19 March 2021

MAGUFULI KUZIKWA MACHI 25

MWILI wa Rais John Pombe Magufuli utazikwa Machi 25 mwaka huu nyumbani kwao Chato, mkoani Geita, ameeleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu wakati alipohutubia taifa punde baada ya kuapishwa.


Rais Samia amesema kuwa kesho Machi 20, 2021 mwili wa Hayati Rais Dk John Magufuli utatolewa Hospitali ya Jeshi Lugalo na kupelekwa Kanisa la St Peter’s Oysterbay, Dar es Salaam kwa Ibada na baadaye utapelekwa Uwanja wa Uhuru kuagwa na viongozi.
-
Machi 21,2021, wananchi wa Dar es salaam watauaga mwili wa
Dk Magufuli na baadaye utasafirishwa kuelekea Dodoma.
-
Machi 22, wananchi wataaga mwili wa Rais Magufuli na kisha utapelekwa jijini Mwanza ambapo Machi 23, utaagwa Mwanza na kisha baadaye kusafirishwa kwenda Chato mkoani Geita.
Machi 24, Mwili wa Hayati, Dk John Pombe Magufuli utaagwa na wanafamilia pamoja na wananchi wa Chato.
-
Machi 25, Hayati Magufuli atafanyiwa maombi katika Kanisa la Katoliki Chato ambapo pia shughuli ya maziko itafanyika baada ya maombi hayo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!