Jiji la Minneapolis katika Jimbo la Minnesota nchini Marekani limefikia makubaliano ya kuilipa fidia Familia ya George Floyd, Mwanaume mweusi aliyefariki akiwa mikononi mwa Polisi Mzungu mwezi Mei mwaka jana.
Mawakili wa Famili hiyo wamesema jiji litailipa USD Milioni 27, ambazo ni nyingi zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya Marekani kama fidia kwa kifo kilichotokea kwa njia za kihalifu.
Polisi anayetuhumiwa kumuua Floyd, Derek Chauvin anakabiliwa na mashtaka ya kuua bila kupanga, ambayo yalinaswa katika mkanda wa video yakidhihirisha uonevu wa kibaguzi uliokita mizizi nchini Marekani.
Wakili wa Familia ya Floyd, Ben Crump amesema ukweli kwamba fidia kubwa zaidi kwa kifo kilichosababishwa na uhalifu imetolewa kwa maisha ya Mtu mweusi, ni ishara yenye nguvu inayotuma ujumbe kwamba maisha ya Mtu mweusi yana thamani nchini Marekani.
( via @dw_kiswahili )
No comments:
Post a Comment