Wednesday, 16 September 2020

Neno la leo- toka kwa Dina Marios!

 

Hakuna mtu anaekuwa na furaha kila wakati lakini kuna namna ya kufurahia maisha japo huzuni au magumu hayakwepeki.

Kinachompa furaha mwanadamu sio hata mali,pesa,mafanikio,watu unaweza ukawa na vyote na bado furaha isiwepo.

La muhumu ni kuappriciate maisha yako.
Maisha kuna wakati yanatuletea vikwazo katika njia zetu.Kuna wakati tunahimili na kuna wakati hatuwezi kuhimili.Pamoja na yote hayo hata wakati upo kwenye changamoto kubwa unaweza kuwa positive ukawa na furaha tu.
Jijali mwenyewe hasa hisia zako,afya yako ya akili na mwili.Kama Kuna wa kusamehewa msamehe tu hata kama hajaomba msamaha.Japo inapendeza na inatua mzigo mtu akikuomba msamaha iwapo amekutendea sivyo.Kwa afya ya moyo na akili yako kama hajaomba huo msamaha muachilie tu msamehe.Mchukulie ni mwanadamu tu ambae ana madhaifu hapo wa muhimu ni wewe.
Kuwa na shukrani...shukuru kwa hali zote hapa duniani hata uwepo wako.Kuwa na shukrani kwa watu hata kwa vitu vidogo walivyokutendea.
Kuwa na Imani...wanasema imani inaweza kusogeza milima.Imani ina nguvu sana.Hata baada ya changamoto unaweza kuvision maisha yajayo unayoyataka.Tengeneza picha na ifanyie kazi kwa imani...njiani utafail amka anza tena mpaka iwe.
Anza leo hii..hakuna muda muafaka...ni sasa hivi.Hata vikwazo vikiibuka buni mbinu ingine ya kufanikisha unayoyataka hasa malengo yako.
Wahudumie wengine kwa furaha,wasaidie,waongoze,kama wakifurahi na wewe unafurahi basi fanya hivyo..Na hiyo ni zawadi kubwa.
Wakati mwingine maisha tusiyachukulie serious sana.Tambua utafanya makosa,utapata majuto,utakosewa pia....Na ipo siku utakufa mwisho utaona unayoyasumbukia utayaacha hapa hapa duniani.
Nenda tu na flow ya maisha usijute muda mrefu,usichukulie mambo serious na usijione muhimu sanaaaa kitu kidogo unakikuzaa.
Pia watambue ulionao...watu wako,familia,marafiki wanaoconnect na wewe ..kumaanisha haupo peke yako unao watu wako.
Kikubwa tafuta sababu ya kufurahi.
Mtumainie Mungu kwa kila jambo...kwake kuna faraja,furaha,hekima,busara,maarifa,matumaini na amani.
Dina Marios.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!