Katika pitapita zangu nimekutana na Post hii daah ni hivi Mtoto huyu kwenye picha anatambulika kwa jina la DORIS AYO , bila shaka MAMA mzazi wa mtoto huyu nadhani anaifahamu vizuri Sura ya mtoto wake kwahiyo akiona picha hii lazima itamgusa .
UJUMBE KWA MAMA DORIS
Sijui ulifikiria nini hadi ukachukua uamuzi wa kumuacha mtoto wako kwa Baba ambaye anamke mwingine , Mtoto wako ulimuacha kwa Baba yake ukadhani umemuacha katika mikono salama kumbe hukujua masikini kama Mtoto wako umemuacha katika mikono ya MTU mwenye roho ya kishetani , Mama Doris hebu tazama kichwa cha mtoto wako kilivyovimba kwa kuchapwa na fimbo angalia mikono ya Mtoto wako ilivyojawa na vidonda pamoja na makovu yaliyotokana na Fimbo daah hii inauma sana jamani . Mama Doris naomba rudi sehemu uliyomuacha mtoto wako ukamchukue mapema vinginevyo utakwenda kuchukua Maiti ya mtoto wako kwahiyo wahi mapema.
Hivi ninyi wamama wa Kambo mnamatatizo gani na kwanini mnakuwa na roho ya kinyama isiyo na huruma sasa faida ya kumtesa mtoto huyu ni ipi au mtoto mdogo kama huyu amekukosea nini wewe ? Hebu muogopeni MUNGU najua sio Mama wa kambo wote mnaroho za kinyama lakini wengi wenu ni wabaya sana Mwenyezi Mungu atawadhibu kwa hilo
BABA DORIS wewe sio Mwanaume sahihi nahisi utakuwa na mapungufu mengi sana kama unaishi nyumba moja na Mtoto wako alafu yanamkuta yote haya na wewe upo hivi utakuwa mzima kweli wewe ? Huyo mwanamke asikudanganye Doris ni damu pia .
Ndugu zangu kama mateso ya Doris yamewagusa naomba #SHARE ujumbe huu katika makundi na akaunti zenu zote ili ujumbe huu umfikie Mama mzazi wa Doris ili akamuokoe mtoto wake kwa maana mtoto yupo katika wakati mgumu sana ahsanteni
No comments:
Post a Comment