Ugonjwa wa figo
Figo ni ogani inayoshirikiana na moyo. Kuathirika kwake kuna athari kubwa kwa mfumo wa damu na mapigo ya moyo.
Magonjwa sugu ya figo hutokea pale ogani hiyo inapopoteza uwezo wa kutenda kazi zake kikamilifu.
Tatizo huanza taratibu na kudumu kwa muda mrefu hadi kuonyesha dalili za wazi .
Huu ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza kwani unatokana na mienendo na mitindo ya kimaisha .
Figo huwa na kazi ya kuchuja takamwili zilizo ndani mwilini na kuzitoa nje kwa njia ya mkojo na kupunguza kiasi cha maji kilichozidi mwilini.
Figo hutoa homoni inayochochea ogani zingine mwilini ikiwamo kuhamasisha utengenezwaji wa chembe nyekundu za damu,utendaji wa madini ya kalsiamu na homoni zinazoongeza mwendo kasi wa misuli ya moyo.
Vilevile ,figo hufanya kazi ya kufyonza na kuvirudisha vitu muhimu ambavyo vingehitajika kutoka kwa njia ya mkojo.
Hudhibiti madini kama potasiumu,magnesiumu,na tindikali ili kuweka sawa mazingira sawia katika damu.
Figo inapopoteza uwezo wake wa kutenda kazi husababisha kukosekana kwa ufanisi wa shughuli za mwili. Hali hii husababisha kuwapo kwa kusanyiko na limbikizo la maji, uchafu na sumu hutokea mwilini mwa mgonjwa.
Pia husababisha kutokea kwa maradhi mengine kama vile, upungufu wa damu mwilini, shinikizo la damu na ongezeko la tindikali kwenye damu. Vilevile husababisha ongezeko la lehemu na mafuta kwenye damu na magonjwa ya mifupa.
Inaelezwa kuwa karibu watu nusu milioni wapo katika uchujaji damu na mashine mbadala wa figo ( dialysis ) na huku wakiwa wameshawahi kubadilishiwa figo.
Mambo kadhaa yanahusishwa na tatizo la ugonjwa sugu wa figo ikiwamo ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu,unene uliopitiliza na uzee.
Vilevile mabadiliko katika tabia na namna watu wanavyohishi.
Ili kujiepusha na hatari ya kupata ugonjwa wa figo fanya yafuatayo.
1. usichelewe kwenda haja
Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya.kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Pia mkojo unaporudi nyuma ya njia husababisha maambukizi katika figo pia njia ya mkojo "nephritis", pamoja na "uremia".
Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya haraka iwezekanavyo nenda kakojoe .
2. kula chumvi kupita kiasi nalo ni tatizo
Inatupasa kula chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku .
3. kula nyama kupita kiasi.
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4.unywaji mwingi wa "caffeines"
Caffeine hutokana na vinywaji vya soda na vinywaji vingine laini kama kahawa, red bull n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza kupata mateso .
Unapaswa kupunguza kiwango cha coke, pepsi, red bull, nk. Ambavyo hunywa kila siku.
5.pia kutokunywa maji
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri .endapo hatunywi maji ya kutosha , sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu ,kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo . Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha nayo ni kuangalia rangi ya mkojo wako,wepesi wa rangi ndiyo vizuri.
6.pia kuchelewa matibabu
Pia epuka vidonge hivi ni hatari sana:-
D- baridi.
Vicks action- 500
Actified
Coldarin
Cosome
Nice
Nimulid
Cetrizet- d
Hivi vidonge vina phenyl propanol- amide ppa ambayo husababisha stroke na zimepigwa marufuku huko marekani.
CRD:Herbalist dr. Mzizimkavu what's app +447459370172
No comments:
Post a Comment