Wednesday, 2 September 2020

“Mamba ana nyama tamu anzeni kula” Naibu Waziri

 

“Mamba ana nyama tamu sana, anzeni kula nyama yake badala ya kutegemea kitoweo cha samaki pekee” ni kauli ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu


Amesema kuwa licha ya nyama hiyo kuwa tamu, lakini kwanza mvunaji wa mamba aombe kibali kutoka kwa maofisa wanyamapori cha kuwavuna kinachotolewa kila Julai Mosi.

“Kuacha nyama yake kuwa tamu, lakini pia ngozi yake ni biashara yenye tija ndani na nje ya nchi” Kanyasu ameeleza kuwa Serikali ina mpango wa kufungua mabucha yatakayouza nyama za wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wizara imeanzisha utaratibu wa uwindaji wa ndani (resident hunting) ambapo nyama zitakazo kuwa zikipatikana zitakuwa zikiuzwa kwenye mabucha hayo,” Kanyasu

“Hivyo wawindaji watatakiwa kufuata taratibu za kuomba vibali kwa ajili ya kuwinda ambavyo vitaainisha aina ya wanyama ambao watakwenda kuwawinda” Kanyasu

MillardAyo.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!